Jumamosi, 19 Oktoba 2013

About Us

About makonelahrecords

Ninafuraha kubwa sana kukujulisha kuwa Makonela Records Inaendelea kutengeneza 'Ngoma' za ukweli, hivyo kama wewe ni msanii na unahitaji au una ndoto ya kutoka kimuziki, basi Makonelah Records ndo suluhisho la kutimiza ndoto yako.

Tunapatikana Zanzibar, Mjini Unguja, katika mtaa wa Mpendae maarufu kama Mchina Mwanzo.

Studio yangu ina historia ndefu katika uandaaji kazi za wasanii, na uzoefu wangu katika 'Production' ni mkubwa na mzuri pia.

Tunaandaa aina zote za muziki, ikiwa ni pamoja na Hip Hop, R&B, Gospel, Taarabu Mchiriku na mingineo mingi.

Kikubwa, kama nilivyosema hapo awali, kwamba tupo Mjini Zanzibar, kwa wakaazi wa Zanzibar na maeneo jirani neno 'Makonela Records' si geni, hususani wanaofuatilia muziki hapa Tanzania na maeneo mengine ambako muziki wa Tanzania unafika.

Piano

Ndani ya Studio yangu katika chumba cha Producer

Vyombo Vya Muziki
Kioo cha kompyuta kikionesha kazi inafanyika

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni